Maelfu ya raia wa Nepal wamelazimika kulala nje kwa siku ya pili
mfulululizo huku barabara zilizofungwa na athari za baada ya tetemeko
zikipunguza kasi ya kuwaokoa manusura.
Karibia watu 2400 wamefariki katika janga hilo ambalo lilikuwa na ukubwa wa 7.8 katika kipimo cha ritcher.
Makundi ya misaada yamesema kuwa kuna uhaba wa umeme na maji huku serikali ikisema kuwa mahema zaidi na vitanda vya muda vinahitajika kwa haraka.
Mwandishi wa BBC katika mji mkuu wa Kathmandu amesema mji uliojaa waathiriwa umeibuka ambapo watu hao wanalala katika mifuko ya plastiki kwa kuwa wanahofu ya kuishi ndani ya majumba yao.
Hata hivyo tetemeko jingine lililotokea jana lilikuwa na ukubwa wa 6.6 katika kipimo cha ritcher
Leo pia limetokea tetemeko la 6,7 katika kipimo cha ritcher na Marekani imeripotiwa kutuma wataalamu wa uokozi kusaidia kuokoa watu waliokwama kwenye vifusi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni