Rais
Uhuru Kenyatta, amewasimamisha kazi wakuu wawili wa shirika
linalopambana na ufisadi nchini humo, siku moja tu baada ya bunge
kupitisha mswaada inaowalaumu kwa uzembe na utepetevu.
Kwa mjibu
wa taarifa kutoka kwa msemaji wa Ikulu ya Rais Manoah Esipisu,tume ya
maadili na kupambana na ufisadi, itaendelea na kazi yake licha ya
kusimamishwa kwa wakuu hao wawili.Waku hao ambao ni mwenyekiti, Mumo Matemu na naibu wake Bi Irene Keino wamesimamishwa huku uchungunzi ukianzishwa dhidi yao kuhusiana na tuhuma za kuzembea kazini na kutumia vibaya mamlaka yao.
Tangazo hilo limefanyika chini ya mwezi mmoja baada ya ripoti kutoka kwa tume hiyo kuwasilishwa kwa Rais Kenyatta iliyosababishwa kusimamishwa kazi kwa mawaziri wanne wa serikali ya Uhuru Kenyatta na maafisa wengine 12 wakuu serikalini, huku uchunguzi dhidi yao ukianzishwa.
Wanatuhumiwa kuhusika na ufisadi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni