Alhamisi, 23 Aprili 2015

BIASHARA YA BINADAMU NI TATIZO KUBWA ULAYA


wahamiaji haramu

Utafiti mpya wa kituo cha Uingereza British Think-Tank unasema kuwa Biashara ya binadamu ni tatizo kubwa linalokumba muungano wa ulaya.

Watafiti katika kituo hicho kinachoshughulikia masuala ya haki za jamii wanasema mafanikio katika vita dhidi ya kile walichokitaja kama biashara ya utumwa mambo leo yamezorota na kwamba mipaka iliyowazi pamoja na internet vimechangia biashara ya binadamu kuwa rahisi.
 
Ripoti hiyo imeelezea namna maelfu ya wanaume na wanawake na watoto wananavyouzwa kwenye mipaka na magenge na kulazimishwa kufanya kazi za ngono, utumwa na uhalifu.

Imetoa wito wa kuwepo kwa juhudi za pamoja za nchi za muungano wa ulaya kukabiliana na tatizo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni