Vikosi
vya usalama nchini Afrika Kusini vimefanya uvamizi kwa usiku wa pili
mjini Johannesburg huku serikali ikijaribu kumaliza ghasia dhidi ya
wahamiaji kutoka mataifa mengine ya Afrika .
Mara hii vikosi vya
usalama vililenga makazi ya wanaume katika kitongoji cha mji wa
Johanesburg cha Alexandra ambako mashambulizi kadhaa dhidi ya wahamiaji
yalifanyika katika wiki za hivi karibuni.Maandamano makubwa ya kudai hatua zichukuliwe kukabiliana na ubaguzi yanatarajiwa kufanyika mjini Johannesburg baadaye hii leo .
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema kuwa ameazimia kushughulikia masuala muhimu yanayosababisha chuki baina ya raia wa nchi yake na wahamiaji
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni