Vijana wakiangalia eneo la mauaji
Serikali ya Kenya inasema kuwa washukiwa watano wa mauaji ya
watu 50 mjini Mpeketoni Pwani mwa Kenya wameuawa.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka katika wizara ya usalama kuhusu
mauaji hayo yaliyofanyika Jumapili usiku na JumatatuTaarifa hiyo pia inasema kuwa silaha nyinginezo zilinaswa.
Shambulizi la pili lilifanyika Jumatatu katika kijiji jirani ambpo watu wengine 9 waliuawa.
Kundi la wapiganaji la Al Shabaab lilikiri kufanya mashambulizi hayo ingawa serikali ya Kenya ilisema kuwa yalichochewa kisiasa. Rais Kenyatta aliwalaumu wanasiasa kwa kuwachochea wananachi pamoja na makundi ya wahalifu kutumia nafasi ya utovu wa usalama kufanya uhalifu(TK).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni