Mtaalamu mashuhuri wa maradhi ya Ki-akili ya dementia ambayo
huathiri uwezo wa kufikiri, Daktari Dennis Gillings, amejitokeza na kuzungumzia
kile anachokiita, mwendo wa Kobe katika taratibu ya kupata tiba mpya ya ugonjwa
huo. Ugonjwa huo wa akili unawaathiri zaidi ya watu milioni 4 kote Duniani.
Daktari Gillings ambaye aliteuliwa na waziri mkuu wa Uingereza mwaka jana
amesema ahadi zilizotolewa na mataifa manene yenye uchumi mkubwa duniani G8
kutafuta tiba ya ugonjwa huo kufikia mwaka 2025 haziwezi kutimizwa bila kuwekeza
zaidi katika utafiti.
Miezi sita baada ya ahadi hizo kutolewa wataalam kutoka maeneo mbalimbali
duniani wanakutana London ili kujadili hatua zinazohitajika kuimarisha utafiti
na majaribio ya dawa za kutibu ugonjwa huo.
Daktari Gillings anasema majaribio ya dawa hizi yanapaswa kudhibitiwa
kuambatana na utaratibu wa majaribio ya dawa zingine.
Serikali ya Uingereza inatarajiwa kuwasilisha ripoti kuhusu ugonjwa huo
nchini humo ambapo watu laki nane wameathirika. Wanasayasi pia watatoa ripoti
itakayoangazia uhusiano wa Ugonjwa wa dementia na lishe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni