Jumanne, 3 Juni 2014

BOKO HARAM YAUA ZAIDI YA WATU 20 KATIKA VIJIJI JIMBO LA BORNO


borno iliyoshambuliwa NIgeria
BBC imepata taarifa kuwa zaidi ya watu 20 wamaeuawa katika mashambulio katika vijiji vya jimbo la Borno.
Hii inatokea wakati bado kuna wasiwasi mkubwa juu ya hatma ya wasichana zaidi ya 200 waliotekwa nyara na kundo hilo yapata siku 50 zilizopita.
Wanadai kuwa walidhania watu hao walikuwa wnajeshi wa serikali waliokuja kuwapa ulinzi. Na baada ya wanajeshi hao kuwafyatulia risasai ndipo waligundua kuwa walikuwa wapiganaji wa Boko Haram.
Mbunge wa eneo hilo Peter Biye amethibitishia BBC tukio hilo na kusema kuwa watu wengi wameuawa na nyumba kuchomwa katika vijiji vingine 5 mbali na hicho.

Jeshi lakanusha madai

Wakati huo huo jeshi la Nigeria limekanusha madai katika vyombo vya habari kuwa mahakama ya kijeshi nchini humo imewapata na hatia baadhi ya maafisa wakuu wa jeshi kwa kuwasaidia wapiganaji wa Boko Haram.
Msemaji kutoka jeshi hilo amekanusha madai kuwa kuna majenerali 15 wa wa jeshi waliofunguliwa mashtaka ya kuwasaidia magaidi.
Jeshi limesema kuwa taarifa hizo ni batili zilizolenga kulidhalilisha jeshi la nchi hiyo wakati mambo yako tete.
nyumba zimechomwa Borno

Hali imeendelea kuwa ya wasiwasi miongoni mwa wakazi wa maeneo mengi kaskazini mashariki mwa Nigeria kutokana na mashambulio yaliyochacha.
Wapiganaji wamekuwa wakishambulia kwa bomu maeneo ya umma na kuwaua watu zaidi ya 200 katika chini ya miezi miwili tu.
Suala la wasichana waliotekwa pia bado limekaa kama mwiba wa samaki kooni mwa serikali ya Nigeria ambapo shinikizo kutoka jamii ya kimataifa zinaendelea kutaka wakombolewe kwa haraka.
Awali serikali ilikuwa imepiga marufuku maandamano yoyote kutokana na tisho la usalama lakini ssa polisi wametangaza kuwa maandamano ya amani yanaweza kufanywa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni