Wachezaji wa Arsenal wakitoka uwanjani vichwa chini baada ya kufungwa goli 3 na Everton
"Lililobaki kwa silimia 100 tutang'ang'ania nafasi ya nne ingawaje ni
vigumu," Wenger amesema.
Wenger ambaye amehudumu katika wadhfa huo katika mechi 1003 amewahi kuingoza
timu hiyo ya Uingereza kufuzu kwa mashindano 16 ya kombe la mabingwa barani
Ulaya.
Shabiki mmoja auliza katika mtandao wa twitter kuwa iweje January walikuwa
nambari moja, february nambari 2, Mwezi wa tatu 3 na sasa mwezi wa nne nambari
nne?
Mwingine asema Bwana Wenger amemtetea kwa miaka mingi - tisa kwa idadi
-lakini leo amekoma.
Amejiunga na wale ambao wameanzisha kampeni katika mtandao Wenger
ajiuzulu.
Kilio cha Arsenal ni furaha ya Liverpool ambao baada ya kuitandika West ham
2-1 wametuliza kileleni mwa ligi
Bashasha sasa pia zasikika katika kambi iliyokuwa imefifia ya Manchester
United baada ya kuimwagia machungu yao yote Newcastle 4- 0 .
Kutokana na Ushindi huo Vijana wa David Moyes hatimaye wameimarika kutoka
nafasi ya 7 hadi nambari 6
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni