Toyota yaagiza magari milioni 6.5 kurejeshwa viwandani
Kampuni kubwa ya uundaji na uuzaji wa magari ya Japan, Toyota i
meagiza magari milioni sita unusu kurejeshwa ilikufanyiwa ukarabati kutokana na
upungufu mbalimbali.
Idadi hiyo ya kurejeshwa magari ni kubwa mno kurejeshwa viwandani.
Kampuni hiyo kubwa zaidi duniani ya uundaji magari inarejesha magari aina ya
Yaris, Urban Cruiser, RAV4 na Hilux.
Kuna hitilafu katika kifuko cha hewa cha kumlinda dereva -(air bag) katika
jumla ya magari milioni tatu, ikiwa haiwezi kuchomoka ili kimlinda dereva wakati
wa ajali.
Aidha kuna hitilafu pia katika baadhi ya viti, usukani na kifaa cha mota ya
kuwasha magari.
Kampuni ya Toyota inasema haijabaini ni ajali ngapi, majeruhi au maafa ambayo
yamesababishwa na matatizo hayo yaliyogundulika majuzi.
Jumla ya magari 20,000 yanahitilafu ya mota ya kuwasha.
Mwezi Februari, Toyota iliagiza magari milioni 1.9 aina ya Prius hybrid
yarejeshwe kutokana na hitlafu iliyopelekea magari hayo kupoteza mwendo
ghafla.
Kwa jumla magari milioni 25 yamerejeshwa katika kipindi cha miaka miwili na
nusu iliyopita.(TK)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni