Serikali ya Kenya imewarudisha nyumbani Wasomali 82 waliokuwa
miongoni mwa wageni 3000 walioshikwa katika msako mkubwa unaoendelea mjini
Nairobi kukabiliana na tishio la ugaidi.
Mwandishi wa BBC mjini Nairobi, Paul Nabiswa, ambaye yuko katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta ameshuhudia zaidi ya Wasomali 82 wakiingizwa
katika ndege moja ambayo imekodishwa maalum kwa shughuli hiyo.
Balozi wa Somalia nchini Kenya , Mohammed Nur amesema kuwa ndege hiyo
imekodishwa na serikali ya Somalia baada ya watu hao kuamua kwa hiari yao
wenyewe kurejea nyumbani baada ya
kukamatwa katika msako unaoendelea mjini Nairobi wakiwa hawana vibali rasmi
ya kuishi nchini Kenya.
Balozi huyo anasisitiza kuwa wasomali wengi wakimbizi walionaswa wakiwa na
stakabadhi rasmi za Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia wakimbizi
UNHCR wataregeshwa katika kambi za
wakimbizi baada ya uchunguzi wa serikali ya Kenya.
Msako huu unaoendelea sasa mjini Nairobi ulianza ijumaa iliyopita baada ya
kutokea milipuko ya grenadi mtaani Eastleigh .
Watu sita waliuawa katika matukio hayo ya mwisho yaliyoibua hasira miongoni
mwa wakenya na kuchochea serikali kuanzisha msako huu.
Kufikia jana Polisi ya Kenya ilidhibitisha kuwa imewanasa wahamiaji 3,000 na
kuwaachilia huku ikiwa imesalia na wahamiaji 447
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni