Timu ya Manchester United jana usiku ilitolewa na bingwa mtetezi Bayern Munic kwa mabao 3 -1 na kutokana na matokeo ya sare ya 1 -1 katika mechi ya kwanza Bayern wanfuzu nusu fainali kwa mabao 4-2. Mechi hiyo ilichezwa nchini Ujerumani na Valencia ndiye aliyefungua mlango wa Bayern kwa kufunga goli safi. Hata hivyo Bayern walirudisha goli hilo na kuongeza mengine mawili kupitia Ribery, Muller na Robben.
Wachezaji wa Man U walishangilia goli lao
Nayo Barcelona ilitolewa na Atletico Madrid baada ya kufungwa goli moja kwa bila. Goli la awali la Koke ndilo lililowaingiza nusu fainali baada ya miak 40.
Mchezaji wa Atletico akishangilia bao hilo pekee kwa mechi hiyo iliyopigwa jana usiku
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni