Jopo
la wataalamu wa serikali ya Marekani limewaagiza wasanifu kuidhinisha dawa ya kutibu
hamu ya kiwango cha chini ya ngono miongoni mwa wanawake inayojulikana
kama ''Female Viagra''.
Wataalam wameiunga mkono dawa hiyo ya Flibarenserin lakini wakasema lazima iwe na onyo la viwango vya juu vya athari zake ikiwemo kuzimia na uchovu.
Uamuzi wa mwisho sasa unaelekea kwa mamlaka inayosimamia chakula na dawa nchini Mareiani FDA.
Mamlaka hiyo imeikataa dawa hiyo mara mbili tangu mwaka 2010 lakini husikiza sana ushauri kutoka kwa wataalam wake.
Wanawake wanaotumia dawa hiyo wameripoti hamu zaidi ya kufanya tendo la ngono,matokeo ambayo wataalamu wanakiri ni ya kawaida.
''Lakini kwa upande mwengine, matokeo ya kawaida yanaweza kusababisha tofauti kubwa iwapo mtumiaji yuko katika hatua fulani za ukaguzi'', alisema daktari Julia Heiman wa taasisi ya Kinsey katika chuo kikuu cha Indiana
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni