Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul akionyesha kifaa kinachotumika na waharifu kwaajili ya kutega barabarani kwaajili ya matukio ya utekaji, alichokamatwa nacho Raia wa Burundi Salvatory Maganga, maarufu kwa kwa jina Nionzima.
Kamanda huyo akionyesha Bunduki aina ya Mark 4 aliokutwa nayo Hashim Ngalawi mkazi wa Mang'ula ambaye pia alikutwa na meno ya tembo mawili.
habari zaidi soma hapo chini
habari zaidi soma hapo chini
MTU mmoja Salvatory Maganga maarufu kwa jina la Nionzima raia wa Burundi ,anashikiliwa na polisi baada ya kupatikana na vitu mbalimbali vya kufanyia matukio ya ujambazi.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Leonard Paul aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, mtu huyo alikamatwa Agosti 31 mwaka huu saa 10.30 katika eneo la Makaburini Mjimpya mansipaa ya Morogoro.
Kamanda huyo alisema jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vya usalama na Raia wema , walibaini mtu huyo kuwa anamiliki vifaa hivyo na kuamua kumwekea mtego na hatimaye kumkamata.
Alitaja vifaa hivyo kuwa ni pamoja na kifaa kilichotengenezwa na vyuma mithiri ya misumari maalumu kwaajili ya kutegea magari barabarani.
Alisema vitu vingine ni visu 10, turubai, darubini, nyaya kufanyia milipuko na bauruti pamoja na mkanda maalumu wa kuvaa tumboni unaosaidia kufanya milipuko hiyo.
Pia alisema mtu huyo alikutwa na kitambulisho cha kupigia kura cha hapa nchini na hati ya kusafiria ya nchini Burundi ambayo inaonyesha miaka ya kuzaliwa tofauti.
Alisema mtu huyo baada ya kufanyiwa mahojiano ya awali alidai alitengeneza vitu hivyo kwaajili ya kutega magari barabarani ili aweze kupata riziki kutokana na maisha yake kuwa magumu.
Hata hivyo kamanda huyo alisema polisi wanaendela na uchunguzi wa kina kujua nia ya rais huyo kukutwa na vitu hivyo hatarishi
Wakati huo huo
JESHI la polisi mkoani hapa limefanikiwa kumkatama Hashim Ngalawi (39) mkazi wa Mang’ula wilayani Kilombero akiwa na bunduki aina ya mark4 na meno ya tembo mawili.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Leonard Paul alisema mtu huyo alikamatwa Agosti 31 mwaka huu, saa 10.45 usiku huko Kanono kisawasawa wilayani Kilombero.
Kamanda huyo alisema mtu huyo anashiliwa na polisi na atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.
Wakati huyo huo Leonard Gaspa anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumporea bastola meneja wa kiwanda cha tumbaku .
Alisema tukio hilo lilitokea Agosti 30 mwaka huu majira ya uskiu wa manane katika eneo la Kahumba manispaa ya Morogoro.
Akielezea mazingira ya kuporwa bastola hiyo kamanda huyo alisema, ilitokea purukushani baina ya watu hao wawili wakiwa ndani ya gari ambapo mtuhumiwa huyo alifanikiwa kupora bastola hiyo na dola za Kimarekani 700 na kasha kutoweka nazo.
Alisema mtuhumiwa huyo alikutwa akitumia dola hizo katika baa mbalimbali mjini hapa na kwamba hadi anakamatwa alikutwa na dola mia moja tu.
Alisema polisi wanaendela na uchunguzi juu ya tukio hilo na kwamba atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni