Tiger
wood amepoteza jino lake la mbele juu baada ya kugongwa na kamera
wakati akimtazama mpenzi wake Lindsey Vonn akinyakua kikombe cha ushindi
Nguli
huyo wa zamani wa mchezo wa gofu, aliamua kwenda katika michuano ya
kuteleza kwenye barafu ili kumshangaza Vonn mpenziwe ambaye alikuwa
hamtarajii kumwona akichuana Cortina d’Ampezzo huko Italia.Baada ya kwisha kwa michuano hiyo ya kuteleza barafuni, watu wakajisogeza karibu na steji ya kutolea tuzo,waandishi ili kutaka kupata picha nzuri wakawa wakisukumana ndipo mwandishi mmoja aliposukumwa na mwenziwe kiasi cha kuteleza kutoka kwenye steji na kamera kumtoka na kumgonga Tiger Woods mdomoni,na wakala ya nguli huyo wa zamani wa mchezo wa golfu alieleza hali hiyo kuwa aligongwa kwa bahati mbaya
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni