Asilimia
50 ya watu wazima nchini Japan hawashiriki katika tendo la ndoa
kulingana na utafiti, swala linalosababisha kupungua kwa idadi ya watu
nchini humo.
Ripoti hiyo iliofanywa na shirika la upangaji uzazi
nchini humo imebaini kwamba asilimia 49.3 ya watu 3000 waliohojiwa
hawakushiriki ndoa mwezi uliopita.Kati ya asilimia 48.3 waliohojiwa walisema kuwa hawakushiriki katika ngono kwa mwezi moja huku asilimia 50.1 ya wanawake wakijizuia kushiriki ndoa. Takwimu zote zilipanda kwa asilimia 5 kutoka kwa ufatiti uliofanywa awali mwaka 2012.
Walipoulizwa ni kwa nini hawashiriki katika tendo la ndoa, asilimia 21.3 ya wanaume walio katika ndoa walidai kuchoka baada ya kutoka kazini huku asilimia 15.7 wakisema kuwa hawana haja ya kushiriki katika tendo la ndoa baada ya wake zao kujifungua.
Kati ya wanawake asilimia 23.8 walisema kuwa tendo la ndoa linasumbua na asilimia 17.8 wakidai walikuwa wamechoka.
Swala jingine la kushangaza ni kuongezeka kwa idadi ya vijana ambao hawana hamu na tendo la ndoa. Zaidi ya asilimia 20 ya wanaume walio kati ya umri wa miaka 25 na 29 hakuwa na hamu ya kufanya ngono ulibainisha utafiti huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni