Mabingwa mara nne
wa kombe la dunia Italia, wameshindwa kufuzu fainali za mwa 2018 nchini
Urusi ikiwa ni mara ya kwanza tokea mwaka 1958 baada ya kutoka suluhu ya
bila kufungana na Sweden.
Hii ina maana kwamba Azzurri watayakosa mashindano hayo kwa mara ya pili tokea kuanzishwa, mara ya kwanza ilikua mwaka 1930.Kiungo Jakob Johansson wa Sweden aliyefunga goli katika mzunguko wa kwanza alikuwa katika kiwango bora na kuwadhibiti vyema Italia katika uwanja wa San Siro.
Wengi walitaraji Italia kushinda mchezo huu kwa sababu lukuki ikiwemo historia sambamba na kucheza nyumbani.
Italia walitawala mchezo kwa asilimia 75 na kupiga mashuti 27 lakini bahati haikuwa upande wao.
Nusura mshambuliaji Stephan El Shaarawy aandike bao kwa upande wa Italia lakini juhudi za mlinda mlango wa Sweden Robin Olsen zilizima ndoto yake.
Matokeo haya yanaifanya Sweden kushiriki mashindano haya tokea mwaka 2006 waliposhiriki kwa mara ya mwisho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni