Jumanne, 20 Januari 2015

AFARKI AKICHEZA MCHEZO WA VIDEO MTANDAONI


Vijana wakicheza michezo mitandaoni ya video
Mtu moja mwenye umri wa miaka 32 huko Taiwan amefariki baada ya kucheza michezo ya mitandaoni,ikiwa ni kisa cha pili kwa mchezaji kama huyo kuaga dunia.
Imebainika kuwa mtu huyo aliaga dunia masaa kadhaa huku wenzake wakiendelea kucheza bila kujua.
Alipatikana amelala katika meza moja ndani ya mgahawa wa mitandao mnamo Januari 8 akiwa hana uhai na kulazimika kupelekwa hospitalini ambapo alitangazwa kwamba amefariki.
Mtu huyo kwa jina Hsieh alikuwa akicheza mchezo huo katika mgahawa wa Kaohsiung,ambao ndio mji wa pili kwa ukubwa nchini Taiwan tangu january 6.
Mtu huyo ambaye hakuwa na ajira alipendelea sana kutembelea migahawa ya mitandao polisi walisema.Inadaiwa kwamba mtu huyo angetoweka kwa siku mbili ama hata tatu kwa mara moja.
Maafisa wa Polisi wamesema kwamba wachezaji wa mchezo wa mtandao katika mgahawa huo waliendelea kucheza bila kugundua ni nini haswa kilichotokea licha ya maafisa hao pamoja na madktari kuwasili ili kumchunguza mtu huyo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni