Jumanne, 20 Januari 2015

MAFUTA MWILINI HUJENGA UBONGO

 
Makalio ya mwanamitindo na mlimbwende Kim Kardashian yamekuwa gumzo kubwa duniani kote
Fumbo la siku zote kwamba wanawake ni wanene kuliko wanaume limepata ufumbuzi...ni wanene kwa wanahitaji mwili wenye umbo zuri na makalio makubwa ili kupata watoto waliojaaliwa werevu.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa wanaakademia ambao wanasema kuwa wanawake wenye makalio na mapaja makubwa na umbo zuri kutokana na mafuta mfano kama Kim Kardashian hupata watoto werevu.
Nini hasa kinawafanya watoto wao kuwa werevu basi? Mafuta yanayopatikana katika sehemu za mwili wa mwanamke huwa na manufaa makubwa sana kwa watoto hasa wanapokuwa wananyonya, mafuta haya hupitia kwenye maziwa ya mama hadi kwa mwili wa mtoto.
Profesa Will Lassek wa chuo kikuu cha Pittsburgh University, Pennsylvania, aliyeongoza utafiti huo, anasema mafuta yanayopatikana katika sehemu hizo za mwili, husaidia sana katika kukuza ubongo wa matoto mchanga.
 
Ubongo wa binadamu
'Unahitaji mafuta mengi ya mwilini ili kuwa na mfumo mzuri wa neva na mafuta katika sehemu hizi za mwili yaani mapaja na makalio, huwa yana madini yajulikanayo kama DHA (docosahexaenoic acid), ambayo ni muhimu sana katika kutengeza ubongo wa binadamu.

Inaonekana kama wanawake wameweza kujua mbinu za kuhifadhi mafuta katika sehemu hizo za mwili hadi wanapopata mtoto.
Kwa muda mrefu haijajulikana kwa nini wanawake wanakuwa wanene sana.......mafuta ya mwili wao yakiwa ni asilimia 30 ya uzani wa mwili.
Professa Lassek anasema kwamba mafuta hayo ni kiwango sawa na yale yanayopatikana katika wanyama kama Dubu au Nyangumi wanapojiandaa kuzaa.
Wanasayansi wanasema mafuta yanayopatikana katika mapaja na makalio ya wanawake ndio yanayotumika kutengeza ubongo wa watoto wachanga.
Mafuta mengi katika mwili wa mwanamke huisha mwilini pindi mama anapomnyonyesha mtoto wake, kulingana na Profesa Lassek, aliyechapisha utafiti wake katika kitabu chake kipya chenye kichwa ''Kwa nini wanawake wanahitaji mafuta mwilini. ''
Wanawake wanaonyonyesha hupoteza kilo nusu ya mafuta mwilini kila mwezi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni