Polisi
katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo, wamefyatua risasi hewani ili
kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wamekusanyika katika mji mkuu
Kinshasa kupinga sheria mpya ya uchaguzi.
Serikali inasema kuwa
watu wanne walifariki katika vurugu za Jumatatu ingawa upinzani unasema
idadi huo huenda ikawa juu kuliko iliyotajwa.Wanafunzi wameweka vizuizi barabarani na pia wameshuhjudiwa wakichoma magurudumu, katika barabara zinazoelekea katika chuo kikuu mjini humo.
Wanatuhumu wanasia wanaomuunga mkono Rais Joseph Kabila ambaye muhula wake wa pili unatarajiwa kumalizika mwaka ujao kwa kujaribu kujiongeza muda mamlakani kwa kuidhinisha mipango ya kufanyika sensa ambayo itachelewesha uchaguzi kwa miaka mingi.
Vurugu hizi zinashuhudiwa huku baraza la Senate likidadisi mswada ambao huenda ukasababisha Rais Kabila kuongezwa muda mamlakani.
Vijana walioandamana kwa vurugugu, waliteketeza magurudumu ya magari, kupora maduka na kurusha mawe.
Wanafunzi waliambia BBC kuwa polisi walivamia chuo chao baada ya wao kuanza kuandamana.
Walisema polisi walingia katika vyumba vyao na kuwafyatulia gesi ya kutoa machozi.
Viongozi wa upinzani walitoa wito kwa waandamanaji kwenda barabarani kupinga mipango ya serikali kumuongeza muda zaidi mamlakani Rais Joseph Kabila huku wakiutaja mpango huo kuwa mapinduzi ya kikatiba.
Mswada huo unapendekeza kufanyika sensa kote nchini ambayo itachukua kipindi cha miaka mitatu.
Rais Kabila amekuwa mamlakani tangu mwaka 2001. Muhula wake wa pili unakamilika mwaka 2016 kikatiba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni