Jumanne, 20 Januari 2015

WAASI WATEKA IKULU NCHINI YEMEN

 
Hali wakati wa makabiliano kati ya waasi na walinzi katika ikulu ya Rais mjini Sanaa
Makabiliano makali yametokea kati ya waasi wa kishia wa Houthi na vikosi vya usalama katika ikulu ya Rais ambao inasadikiwa waasi hao wameiteka ikulu ya Rais.
Walioshuhudia makabiliano hayo wanasema waasi hao walipambana na vikosi vya usalama kwa muda kabla ya kuingia katika ikulu ya Rais.
Awali, Rais Abd Rabbuh Mansour Hadi alifanya mazungumzo ya dharura na washauri wake siku moja baada ya vifo vya watu tisa kufuatia makabiliano mengine kati ya waasi hao na wanajeshi mnamo Jumatatu.
 
Waasi wa Houthis
Makubaliano yalifikiwa lakini waasi wa Houthis waliendelea kuzingira ikulu ya Rais na makao ya waziri mkuu.
Kiongozi wa waasi hao anatarajiwa kutoa hotuba baadaye leo wakati baraza la usalama la Umoja wa Mataifa likijiandaa kwa mkutano wa dharura kujadili hali nchini Yemen.
Kanali Saleh al-Jamalani, ambaye ni mkuu wa kikosi cha ulinzi wa ikulu ya Rais Abed Rabbo Mansour Hadi, ameambia shirika la habari la AP kwamba waasi hao walivamia ikulu nyakati za mchana.
Rais Hadi inaarufiwa hakuwa katika makao hayo wakati waasi walipoivamia ikulu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni