Mwanamume mmoja amekiri kumchinja na kisha kumkatakata mkewe katika nyumba yao mjini London.
Naveed
Ahmed, mwenye umri wa miaka 41, alikiri makosa yake ya kumuua mkewe
ambaye ni mama wa watoto wake wawili, Tahira Ahmed, 38.Mwili wa Bi Ahmed ulipatikana na polisi tarehe 27 mwezi Mei baada ya majirani kuripoti kwamba walisikia wawili hao wakigombana.
Uchunguzi wa kifo chja mwanamke huyo ilisema kuwa alipatikana akiwa amekatwa mikono , kudungwa kisu na kisha kukatwakatwa
.
Bwana Ahmed anatarajiwa kuhukumiwa tarehe 28 mwezi huu katika mahakama aya Old Bailey.
Inaarfiwa jaji amemuonya kwamba huenda akafungwa jela kwa mauaji hayo.
Awali Ahmed alikana mauaji ya mkewe wakati kesi ilipoanza kusikilizwa mwezi Oktoba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni