Utawala
nchini Malawi unasema kuwa umewaokoa maelfu ya watu ambao walikuwa
wamekwama kutokana na mafuriko ambayo yameikumba nchi hiyo.
Wanajeshi
walitumia mashua na ndege za helikopta kuwahamisha watu kwenda maeneo
yaliyoinuka kufuatia kuharibiwa kwa barabara na madaraja.Takriban watu 200 wameripotiwa kuaga dunia huku wengine 200,000 wakilazimika kuhama makwao.
Serikali ya Msumbiji imeomba msaada wa kimataifa ambapo pia imeweka kambi ikiwa inawapa waathirika chakula maji na makao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni