Aliekuwemo kwenye hili basi ndio amenitumia hizi picha na kuniambia watu wanne wamefariki dunia na 34 kujeruhiwa baada ya basi lao kuanguka katika eneo la Mkange Berega. Basi linaitwa Air Bus na limepata ajali likielekea Dodoma kutokea Morogoro baada ya kifaa cha usukani kushindwa kufanya kazi ambapo muda mfupi baadaye anasema alisikia tu dereva akipiga kelele na kisha kikafuataiwa na kishindo, basi likaacha njia na kwenda bondeni. Ajali hii imetokea siku tatu baada ya Waziri wa uchukuzi Dr. Harryson Mwakyembe kufungia kampuni mbili za mabasi ya J4 Express na Mwanza Coach yaliyogongana na kuua 39 Musoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni