Jumanne, 9 Septemba 2014

NYAMA YA KIBOKO YAUA HUKO NCHINI DRC

Nyama ya Kiboko huliwa na watu wengi

Watu kumi waliuawa na gari lililokuwa linakwenda kwa mwendo wa kasi walipokuwa wanajaribu kujipatia angalau kipande cha nyama ya Kiboko mwishoni mwa wiki.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa mtandao wa Daily Nation.

Kiboko huyo alikuwa amegongwa na gari na kufa Jumamosi jioni katika mkoa wa Limpopo wakati ambapo wanakijiji walikimbia katika sehemu hiyo angalau kujipatia kipande cha nyama.

Msemaji wa polisi aliliambia shirika la habari la AFP kwamba mnyama huyo aligongwa na ndipo wanakijiji wakaona kuwa ni fursa ya kupata nyama ya bure ambapo walikimbia kuichukua na kuanza kuikatakata, ''

''Hapo ndipo gari lililokuwa linakwenda kwa kasi liliwagonga watu 8 walipokuwa wanakata nyama hiyo na kuwaua papo hapo,'' aliongeza kusema msemaji huyo wa polisi.

Watu wengine wawili walifariki kutokana na majereha yao mabaya wakiwa wanapatiwa matibabu hospitalini.

Polisi wanasema kuwa watu wengine saba akiwemo dereva wa gari hilo wanapata matibabu hospitalini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni