Pwani ya Sicily nchini Italia
Zaidi
 ya watu 40 wamekufa maji katika pwani ya Sicily nchini Italia huku 
serikali ya taifa hilo ikitoa wito wa msaada zaidi kutoka kwa muungano 
wa Ulaya kusaidia kusitisha ongezeko la wahamiaji wanaovuka bahari ya 
shamu.
Watu wanne wanadaiwa kunusurika baada ya boti yao kuzama.
Karibia wahamiaji 10,000 wameokolewa wakijaribu kuelekea katika pwani ya Itali katika siku za hivi karibuni.
Mamia wamekufa maji tangu mwanzo wa mwaka huu.
Wito huo unajiri huku waziri wa maswala ya kigeni Paolo Gentilon akisema kuwa Itali haijapata usaidizi wa kutosha kutoka kwa Muungano wa Ulaya
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni