Alhamisi, 23 Februari 2017

Sayari saba mpya sawa na Dunia zagunduliwa

Sayari zingine saba zagunduliwa anga za mbali

Sayari zingine saba zagunduliwa anga za mbali
Wataalamu wa masuala ya anga za juu wa Marekani wakishirikiana na wengine duniani, wamefanya ugunduzi mkubwa wa sayari saba zenye ukubwa sawa na wa Dunia ambazo zinaizunguka nyota mojawapo kama ilivyo kwa dunia kulizunguka jua.
Wanasayansi hao wa anga za mbali kutoka Marekani, Uingereza na Ubelgiji, wamebainisha kuwa sayari hizo saba walizozigundua zinaizunguka nyota ijulikanayo kwa jina la Trappist One.
Hata hivyo wanasayansi hao wamesisitiza kuwa kwa teknolojia iliyopo sasa inaweza kuwachukua maelfu ya miaka kuzifikia sayari hizo.


Thomas Zurbuchen kutoka shirika la NASA lenye makao yake makuu Washington nchini Marekani, amewaambia waandishi wa habari kuwa haya ni mafanikio hayo ni makubwa kisayansi na yanajibu maswali makubwa ya kisayansi
"Ugunduzi huu unatupatia vidokezo muhimu vya kuitafuta 'dunia ya pili', na kwamba sasa si jamba la kusema kama ingelikuwa hivi, bali sasa tunasema ni lini. Wanasayansi wanaamini kwamba takribani katika kila nyota moja kuna uwezekano wa kuwepo sayari moja. Chukulia sasa nyota tatu, nne, tano hadi saba, jiulize ni idadi ya dunia ngapi zilizopo pale,'' amesema Zurbuchen.
SayariHaki miliki ya picha Nature
Michael Gillion ni mmoja wa wanajopo hilo la wana sayansi kutoka chuo kikuu cha anasema sayari tatu kati ya hizo saba zilizogundiliwa zipo karibu na nyota hiyo na zina sifa tofauti.
"Inaonesha kuwa sayari hizi tatu kati ya hizo saba zilizogunduliwa zipo katika ukanda unaoweza kuruhusu viumbe kuishi, kwani maji yanaweza kupatikana na maisha ya viumbe hai yanaweza kuendelea, chakushangaza zaidi ni kwamba maisha yanaweza kuwepo hata katika uso wa sayari hizo," amesema Gillion.
Ugunduzi huu unatajwa na wanasayansi hawa kuwa ni mafanikio makubwa na umewaingiza katika ukurasa mwingine na kubakiwa na swali moja tu kwamba ni lini watazifikia sayari hizo badala ya kujiuliza kuwa katika sayari hizo kuna nini.
  Poster
NASA imetoa bango la "kusafiri" kwenda kwenye mfumo huo wa nyota
Hata kuzifikia sayari hizo ni mtihani mwingine wani umbali wake hata mwendokasi wa mwanga, unaoongoza hapa duniani kwenda kwa haraka, unaweza kuzifikia sayari hizo baada ya miaka 40.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni