Serikali ya Jimbo la Kashmir nchini India imeweka zuio dhidi ya gharama za anasa.
Wazazi wa bibi harusi watapigwa marufuku kualika zaidi ya wageni mia tano, na wazazi wa bwana harusi watapigwa marufuku kualika zaidi ya watu mia nne.Idadi ya aina ya vyakula kwenye sherehe itakuwa saba, huku mziki wa sauti ya juu na fataki vitapigwa marufuku.
Serikali ya Kashmir imesema imechukua hatua hiyo baada ya kuwepo kwa malalamiko ya watu kuhusu matumizi makubwa wakati wa sherehe na kelele zinazowakera wengine.
Amri hizo zitaanza kufanya kazi mwezi Aprili 2017.
Hapa Tanzania harusi zinakuwa na watu hata 1000 huku michango ya harusi ikifikia milioni 50 hadi 60 na kuendelea.
Jambo hili linawakera watu wengi hasa ukuzingatia kuwa fedha yote hii inaliwa kwa siku moja tu huku watu wakishindana ni shughuli ya nani ni kubwa zaidi. Serikali ingeiga mfano wa Kashmir au kwenda zaidi ya hapo ingefanya la maana sana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni