Huu ni mji wa milimani nje ya mji wa Belo Horizante ambao unaongzwa na kinamama pekee.Mji huu una wakazi wapatao 600 wengi wao wakiwa hawajaolewa na wenye miaka 20 na 25. Watoto wa kiume wakifikia miaka 18 wanaondolewa na wanaume waliooa humo wamepigwa marufuku kukaa humo mpaka wikiendi tu.
Kwa sasa wanawake hao wameomba serikali iwaletee wanaume lakini wafuate sheria za mji huo.
Mji huo ulianzishwa mwaka 1891 na Maria
Senhorinha de Lima, ambaye alitengwa na Kanisa mwa uzinzi baada ya kumuacha mumewe ambaye alikuwa amemuoa kwa nguvu. Baada ya muda wanawake wengine walijiunga naye Mwaka 1940, mchungaji wa kievanjelist, Anisio Pereira, alimchukua msichana mmoja wa wasichana wa mji huo kama mke na akaanzish kanisa na kuweka sheria ngumu. Alipokufa mwaka 1995, waliapa kutorudia tena kosa la kuongozwa na kuvunja kanisa la Pereira's.
Mkazi mmoja wa mji huo Nelma Fernandes, 23, alisema, "wanaume pekee tunaokutana nao sisi ni waume wa watu au ndugu zetu. Wote tunatamani kuwa na waume zetu . Lakini tunaishi hapa na hatuhitaji kuondoka mji huu ili kutafuta wanaume. Mwanamume anayetaka kuja huku aje lakini akubali kufuata sheri zetu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni