Idris akionekana ni mwenye furaha kubwa sana baada ya kuwasili nchini.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Barbara Kambogi
(kati) akijadiliana jambo na Mshindi wa Big Brother Africa 2014,Idris
Sultan pamoja na aliekuwa mshiriki wa shindano hilo,Laveda katika uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa Shindano la Big Brother Africa 2014, Idris Sultan,
akizongwa na umati wa watu mashabiki wake huku akiwa na furaha baada ya
kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Idris
ameibuka kidedea na kunyakua taji hilo la Big Brother Africa 2014.
Kushoto kwake ni Laveda aliekuwa mshiriki mweza wa Idris.
Mshindi wa Big Brother Africa 2014,Idris Sultan, akizungumza wakati akihojiwa na waandishi wa habari, baada ya kuwasili nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni