Alhamisi, 5 Machi 2015

WATU WANNE KUNYONGWA HADI KUFA MWANZA


Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete

Mahakama kuu ya Tanzania Mwanza imewahukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa washtakiwa wanne akiwemo mume wa marehemu baada ya kupatikana na hatia ya kumuua zawadi Mangidu [22] wa kijiji cha Nyamalulu kata ya Kaseme wilayani Geita.
Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Joaquine De-Mello katika ukumbi uliokuwa umefurika wasikilizaji wakiwemo ndugu wa upande wa washtakiwa na baada ya kutolewa hukumu baadhi ya ndugu wa washtakiwa walitokwa na machozi
Waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa ni Masalu Kahindi[54]Ndahanya Lumola[42]Singu Nsiyantemi[49]na Nassor Said[47] ambaye alikuwa mume wa marehemu Zawadi Mangindu wote wamepatikana na hatia ya kula njama na kushiriki kumuua zawadi kwa kukusudia ambaye alikuwa mlemavu wa ngozi.
Katika hukumu yake Jaji De-mello alisema alikuwa amezingatia kwa makini na tahadhari kubwa katika kufikia uamzi huo baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka ambapo mashahidi 12 waliitwa na kutoa ushahidi pamoja na ule wa Utetezi na kisha kujiridhisha kuwa pasipo kuacha shaka yoyote washtakiwa walitenda kosa hilo.

Aliongeza kuwa katika hukumu zilizotangulia pia zimebainisha kuwa mauaji ya walemavu wa ngozi yamekuwa yanatekelezwa na mtandao mkubwa na siyo rahisi kuubani bila umakini na kuomba katika kesi zijazo pia wanunuzi wa viungo na wagangawanaopiga ramili nao wafikishwe mahakamani kwani uzoefu unaonyesha wauaji hufikishwa mahakamani kwani nao ni wauaji.
Huku wasilikizaji wakifuatilia kwa umakini hukumu hiy wakati akiisoma Mheshimwa Jaji De-mello aliisisitiza kuwa Ushahidi uliotolewana Magdalena Shimba mama mzazi wa marehemu na shahidi Semeni [14]waliothibitisha mahakamani kuwaona na kuwatambua washtakiwa wa kwanza na wanne kwenye eneo la tukio pamoja na mazingira yaliyoelezwa mahakamani yanaifanya mahakama pasipo kuacha shaka yoyote.
Awali upande wa Mashtaka wakati ukiongozwa na wakili wa serkali Hezron Mwasimba akisaidiana na wakili Janeth Kisibo ulidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa kwa pamoja kwa makusudi walishirikiana kula njama na kutenda kosa la kumuua Zawadi Mangidu[22] aliyekuwa mlemavu wa ngozi hapo Machi 11 mwaka 2008 saa moja usiku katika kijiji cha Nyamalulukata ya Kaseme Wilayani Geita walitenda kosa hilo na pia kumjeruhi mtoto Chausiku aliyekuwa na umri wa miezi 9 wakati huo kwa panga katika mkono wake akiwa mtoto wa mareheu.
Upande wa mashtaka uliendelea kudai washtakiwa walikamatwa kwa nyakati tofauti baadaye na taratibu za kisheriazilizingatiwa ikiwemo kupewa nafasi ya kutoa maelezo ya onyo na kutoa Ungamo na baadaye walifikishwa mahakamani ambapo Jamhuri iliwezakuita mashaihdi 12 na kutoa ushahidi hivyo kuiomba mahakama kuu kutoa adhabu kali kwa washtakiwa ili kuwa fundisho kwa watu wengine aina hiyona kuwa ilidaiwa viungo hivyo hutumiwa kuwawezesha watu kupata utajiri ikiwemo wa madini.
Hata hivyo wakati wa kesi hiyo malumbano makubwa yalitokea wakati upande wa utetezi ukipinga maelezo ya Ungamo na Onyo kutopokea kama kilelelezo na mahakamawkwa madai wastahkwia walishinikizwa kukiri maelezo hayo hatua iliyomfanya Jaji kuingilia kwa kusema kuwa mazingira ya yaliyochukuliwa maelezo hayo ya ungamo na Onyo yanaashiria washtakiwa hawakulazimishwa hivyo mahakama kuu kuyapokea kama sehemu ya ushahidi.

Rais Kikwete akizungumzia mauaji ya albino
Wakati kesi hiyo ilidaiwa na upande wa mashatka kuwa washtakiwa wanadaiwa kuchukua kiasi cha shilingi 250,000 kati ya shilingi 1,250,000 kutoka kwa wakala wa kununua viungo hivyo baada ya kuvifikisha ilibainika viungo vya marehemuhavikuwa na kiwango cha ubora unaotakiwa hivyo Wakala wao alikataa kumalizi a kaisi cha shilingimilioni 1 kilichokuwa kimebakia ambaye alitajwa mahakamani kwa jina la Hamis Hamad mkazi wa mkoani Shinyanga ambaye hakuweza kupatikana.
Ilidaiwa kuwa baada ya mlemavu wa ngozi kuuawa viungo vyake hufanyiwa utambuzi wa ubora wa viungo vyake ambapo wembe,radio na sarafu ya shilingi kumi hutumiwa katika kutambua ubora wake na kiungo kikigusishwa kwenye radio ,radio hukwaruza kwa kupiga kelele na hata kuzima ubora huo ndio unaotakiwa lakini kisipotoa ishara hizo basi kinakuwa hakina kiwango cha ubora unaoatakiwa hakihitajiki.
Jaji De-mello alihitimisha kwa kuamru washtakiwa kunyongwa hadi kufa ,..na haki ya kukata rufafa ilkuwa wazi kwao hivyo kuufanya ukumbi mzima kukaa kimya na baada ya kutoka nje ya ukumbi wengi walijitokeza kuunga mkono hukumu hiyo,na imekuja huku kukiwa na tukio la mtoto Yohana bahati naye kuuawa mkoani humo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni