Mtoto Hassan Khamis ni miongoni mwa walemavu wa ngozi wanaohifadhiwa
kwenye kituo cha Buhangija nchini Tanzania na sasa akiwa ameshakuwa
mkubwa na kulazimika kutoka hapo, anasema hana uhakika wa maisha yake.
Katika mfululizo huu wa ripoti maalumu mwezi mzima kuangazia masaibu,
changamoto na maisha wanayopitia watu wenye ulemavu wa ngozi, maarufu
kama albino, ambao hivi karibuni wamekuwa wakilengwa na kushambuliwa
nchini Tanzania kwa imani za kishirikina, hapa Idhaa ya Kiswahili ya DW
inazungumza na kijana Hassani mwenye umri wa miaka 17 sasa na ambaye
amehifadhiwa katika kituo cha Buhangija kinachowashughulikia watu
wanaoishi na ulemavu wa ngozi mjini Shinyanga, Tanzania.Kusikiliza mahojiano na kijana Hassani, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Amina Abubakar
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni