BOKO HARAMWAKIRI KUTEKA WASICHANA ZAIDI YA 200 NIGERIA
Wasichana waliotoroka
mikononi mwa Boko Haram
Kiongozi wa Boko Haram
Abubakar Shekau.
Kundi la kislamu nchini
Nigeria la Boko Haram linasema kuwa ndilo lililowateka nyara zaidi ya wasichana
wa shule 200 ambao hawajulikani waliko kwa wiki tatu sasa.
Kupitia kwa njia ya
video kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau amesema kuwa watawauza wasichana
hao. Wasichana hao walitekwa kutoka shule moja iliyo kaskazini mashariki mwa
nchi.
Wakati huo mwanamke ambaye ni kiongozi wa maandamano
nchini humo Naomi Mutah aliyekuwa ameshikiliwa na polisi kwa amri ya mke wa rais
wa nchi hiyo Patience Jonathan amechiwa huru.
Kumekuwa na shinikizo kwa serikali ya nchi hiyo kwamba
haijafanya juhudi kubwa kuwaokoa wasichana hao.
Akizunguma kwa mara kwa kwanza rais wa Nigeria Goodluck
Jonathan amesema kuwa atafanya kila awezalo kuwakoa wasichana hao.
Wazazi wa wasichana hao
wakilia
Waandamanaji wakitaka serikali ichukue hatua kuwaokoa
wasichana hao.BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni