Jumatatu, 5 Mei 2014

WAHABESHI 55 WANASWA HIMO MOSHI


Waethiopia 55 wamekamatwa na wanakijiji cha Chekereni Pabliki kilichopo Himo, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wakiwa wamejificha kichakani na mkazi mmoja wa kijiji hicho.
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz, amethibitisha kutokea tukio hilo na kwamba watu hao walikamatwa
“Wanakijiji walitoa taarifa polisi baada ya kuwaona watu hao, na sisi tulifika mara moja kuwakamata wakiwa na mwenyeji wao,” alisema Kamanda Boaz.
Aliongeza: “Kwa sasa hatuwezi kumtaja jina wenyeji wa watu hao kwa vile bado tunaendelea na uchunguzi zaidi.”
Kwa mujibu wa Kamanda Boaz, watu hao baada ya kuhojiwa walidai kuwa walikuwa njiani kwenda nchini Afrika Kusini kupitia Tanzania.
Alisema uchunguzi unaendelea ili kubaini wahusika wengine zaidi wa mtandao wa kusafirisha binadamu kabla ya kufikishwa mahakamani.
Aliwataka wananchi waishio mipakani kuendelea kuwa walinzi na kutoa taarifa polisi pindi wanapowaona watu wanaowatilia shaka katika maeneo yao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni