Manchester United ilikosa fursa ya
kupanda juu na pointi kumi dhidi ya Liverpool baada ya kulazwa mabao
matatu bila na kilabu ya Everton.
United wangeongeza mwanya uliopo kati yao na Liverpool katika kinyanganyiro cha kufuzu katika kombe la vilabu bingwa Ulaya.Lakini mabao ya James Mc Carthy na John Stone yaliiweka Everton kifua mbele kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.
Kelvin Mereiles aligonga msumari wa mwisho katika jeneza la United alipofunga bao la tatu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni