Wanafunzi wa kike watekwa nyara Nigeria
Polisi nchini Nigeria wanasema kuwa shule ya mabweni ya
wasichana imeshambuliwa katika jimbo la Borno Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo
huku wasichana wakitekwa nyara.
Shambulizi hili linadaiwa kufanywa na Boko Haram ingawa kundi hilo halijakiri kulitekeleza
Wazazi wanasema kuwa zaidi ya wasichana mia moja wametekwa nyara na
washambuliaji hao.
Washambuliaji wanaaminika kuwa wanachama wa kundi la wapiganaji wa kiisilamu
la Boko Haram. Utekaji nyara huo ulifanyika usiku wa manane katika shule ya
Chibok Kusini mwa mji wa Borno, karibu na mpaka na Cameroon.
Inaarifiwa wasichana 300 walikuwa wanajiandaa kwa mitihani yao. Mmoja wa
wasichana alifanikiwa kutoroka na aliambia BBC kuwa walikuwa wanalala wakati
walipovamiwa na wanaume waliokuwa wamejihami.
Waliowashambulia wanaaminika kuwa wapiganaji wa kundi la Boko Haram.
Wanaume hao waliingiza magunia ya chakula katika malori yao na kuwaamuru
wasichana kupanda lori hizo.
Wasichana 15 walifanikiwa kutoroka baada ya lori walimokuwa kukumbwa na
hitilafu.
Wakazi wa kijiji cha Chibok wanasema kuwa walisikia milipuko kadhaa huku
nyumba 170 zikiteketezwa.
Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa wanajeshi wawili waliuawa huku
mali ikiharibiwa wakati wa shamblizi hilo mjini Chibok.
Mnamo siku ya Jumatatu, zaidi ya watu 70, waliuawa katika milipuko miwili ya
mabomu katika kituo cha mabasi mjini Abuja.
Kundi la Boko Haram pia limelaumiwa kwa kufanya shambulizi hilo (TK)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni