Sokwe hawa wa milimani wanakabiliwa na tisho la kutoweka
kutokana na kuwindwa sana
Mmoja wa viongozi wakuu wa uhifadhi wa wanyama pori barani
Afrika Emmanuel de Merode, amejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa risasi na watu
wasiojulikana katika moja ya mbuga kongwe barani afrika.
Bwana Merode,ambaye ni raia wa Ubelgiji ni mkurugenzi wa mbunga ya wanyamapori ya Virunga, ambayo ni makao ya Sokwe wanaokaa milimani katika Jamuhuri ya
kidemokrasia ya Congo.
Sokwe hao ni baadhi ya wanyama walio katika hatari ya kutoweka kutokana na
kuwindwa sana.
Alipigwa risasi akiwa anaendesha gari kati ya eneo lililo kati ya makao makuu
ya mbuga hiyo na mji wa Goma ambako amelazwa hospitalini.
Sababu ya kupigwa risasi kwa mhifadhi huyo haijajulikana, lakini makundi ya
watu ambao hukata miti kiharamu, wawindaji haramu na waasi huendesha shughuli
zao katika eneo hilo -BBC (TK)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni