Watu walionusurika wamekuwa wakielezea hali ilivyokuwa ya
kutisha ndani ya meli ya Korea Kusini ilipoanza kusimama kwa kuyumba, akiegemea
upande mmoja na haraka kuanza kuzama.
"Kwa kweli kulikuwa na sauti kubwa na meli ghafla ikanza kuegemea upande
mmoja," amesema abiria aliyeokolewa, Kim Song-Muk.
Meli ya Korea Kusini ikizama kulia
"watu walikuwa wakihangaika kukimbilia maeneo ya juu ya meli, lakini ilikuwa
vigumu kufanya hivyo kutokana na meli kupinduka."
Bado haijafahamika kilichosababisha kuzama kwa meli hiyo, ambayo kwa kiasi
kikubwa iliwabeba wanafunzi wa shule, lakini watu walionusurika katika ajali
hiyo wanatoa maelezo sawa kuhusu tukio hilo la kutisha.
Kikosi cha Walinzi wa Pwani ya Korea Kusini kimesema abiria wapatao mia tatu
hawajulikani walipo baada ya meli kupinduka na kuzama.
Mtu mmoja wamethibitika kupoteza maisha na watu mia moja na sitini na wanne
wameokolewa. Kikosi cha wapiga mbizi kwa sasa wanatafuta meli iliyozama. Wengi
wa abiria wa meli hiyo ni wanafunzi wa sekondari wakiwa katika safari ya masomo
kuelekea kisiwa cha Jeju, nchini Korea Kusini.
Meli hiyo ilikuwa na watu 460
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni