Waasi wadai kuudhibiti upya Bentiu kutoka kikosi cha
serikali
Wapiganaji nchini Sudan Kusini wanasema wameudhibiti mji mkubwa
katika jimbo lenye utajiri wa mafuta, na wametoa makatazo kwa makampuni ya mafuta
kusitisha uchimbaji wa mafuta na iwaondoshe wafanyakazi.
Walinda amani wa Umoja wa mataifa waliwaokoa wafanyakazi kumi wa kampuni ya
mafuta ya Urusi, Safinat kaskazini mwa mji wa Bentiu, kutoka ghasia hizo, watano
kati yao walijeruhiwa.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka jimbo la Unity, kamanda mmoja wa waasi
alieleza kwamba kikosi cha waasi kimeudhibiti upya mji wa Bentiu kutoka kwa
wanajeshi wa serikali.
Sudan kuisni imeshuhudia ghasia kubwa mnamo mwezi Desemba, wakati kulizuka
mapigano kati ya wanajeshi wanaomtii aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar na
wale wanaomtii rais Salva Kiir.
Maelfu ya watu wanaaminika kuuawa huku wengine zaidi ya milioni wakiyakimbia
makaazi yao.
Raia wengi wametoroka makaazi yao kutokana na mapigano
Wakati mapigano hayo yanaendelea mratibu wa misaada wa Umoja wamataifa nchini
humo, Toby Lanzer, ameghadhabishwa na kukasirishwa na viongozi wa kisiasa na
kijeshi Sudan kusini.
Amesema kuzuka upya mapigano hayo kutaathiri jitihda za kuepuka baa la njaa
linalotarajiwa.
Maafisa wa mashirika ya kimataifa ya misaada wametumia 'baa la njaa' mara kwa
mara kuelezea hali itakayoikabili Sudan kusini katika miezi ijayo.
Nchi hiyo ni maskini na wakazi wengi wanaishi kwa kula vyakula wanavyopanda
na kuvuna. Kutokana na mapigano yanayoendelea, wakazi wengi wanashindwa kupanda
vyakula kwa matayarisho ya msimu ujao wa mvua (TK).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni