Mkuu
wa utawala wa waasi nchini Libya ameiambia BBC kuwa vikosi vyao
vinafanya juhudi ziwezekanazo kuzuia wahamiaji haramu kuabiri meli
kuelekea Ulaya .
Khalifa Al-Ghwell - ambaye serikali yake ya
uokozi yenye makao yake mjini Tripoli haitambuliwi kimataifa anasema
walinzi wa Libya wa mwambao wamekuwa wakiwashikilia karibu wahamiaji mia
nne - kutoka nchi za Sahara barani Afrika katika kipindi cha siku
chache zilizopita .Bwana Ghwell amesema kuwa wahamiaji elfu 17 walikuwa wanaishi katika kambi ya hifadhi nchini Libya , lakini ni asilimia karibu tano walioweza kuvuka na kuingia Ulaya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni