Jumanne, 3 Machi 2015

LESOTHO KUUNDA SERIKALI YA SHIRIKISHO?

Lesotho yajiandaa kuunda serikali ya muungano

Waziri mkuu wa Lesotho, Thomas Thabane, akipokelewa na wafuasi wake, katika mji mkuu wa Lesotho, Maseru, Februari 26 mwaka 2015.
Waziri mkuu wa Lesotho, Thomas Thabane, akipokelewa na wafuasi wake, katika mji mkuu wa

Lesotho inaelekea kuunda serikali ya muungano kutokana na kile kinachoonekana kuwa hakuna atakayepata ushindi wa moja kwa moja katika Uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa juma lililopita.

Hadi sasa chama cha Waziri Mkuu Thomas Thabane cha All Basotho Convention kinaongoza na tayari kimepata viti 40 vya ubunge ikilinganishwa na chama cha Waziri Mkuu wa zamani cha Democratic Congress ambacho kina viti 33.
Mshindi anahitajika kupata ushindi wa viti 61 kati ya 120 ili kuweza kuunda serikali bila ya kushirikiana na chama kingine.
Wachambuzi wa siasa nchini humo wanasema matokeo yanaonesha wazi kuwa uwezekano ni mkubwa wa kuundwa kwa serikali ya muungano.
Waangalizi wa Uchaguzi huo wanasema, zoezi hilo limekuwa huru na haki na wananchi wa Lesotho walipiga kura kwa amani.
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga ambaye anaongoza waangalizi wa Umoja wa Afrika licha ya kuusifu uchaguzi huo kuwa huru na haki ameonya kuwa huenda kukatokea na mvutano kati ya jeshi na polisi katika nchi hiyo ikiwa mkataba wa kutoingilia siasa hautaheshimiwa.
Matokeo ya mwisho yatafahamika kesho Jumatano katika taifa hilo la Kusini mwa Afrika ambalo lililazamika kuandaa uchaguzi huo kutokana na jaribio la kuipundua serikali mwaka jana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni