Nchi nne zinachangia ziwa Chad : Chad, Cameroon, Niger na Nigeria.
Idadi ya watu waliouawa katika mashambulizi hayo bado ni ya
muda, lakini kwa mujibu wa mashahidi katika vijiji hivyo, watu tisa kwa
uchache waliuawa.
Wanamgambo wa Boko Haram waliingia katika vijiji hivyo wakitumia mitumbwi kwenye saa mbili usiku Jumapili Machi 1, na kuanza kushambulia kwa risasi na vilipuzi katika nyumba mbalimbali za vijiji hivyo.
Katika kisiwa cha Kui Keleha, watu wawili waliuawa, na wengine walichomwa moto ndani ya nyumba zao, na wengine tena walikufa maji wakati wakijaribu kuokoa nafsi zao, kama alivyothibitisha, El Adj Aboubacar, mbunge wa Bosso.
“ Walichoma moto watu tisa kwa wakati mmoja, na mtumbwi uliyokuwa ukiwasafirisha wanawake na watoto, ambao walikuwa wakijaribu kuokoa maisha yao ulizama ziwani. Watu wanane walifariki dunia", amesema El Adj Aboubacar.
Kwa uchache watu 19 walifariki baada ya shambulio lililoendeshwa katika vijiji vya Kui Kaleha na Toumbu Buka, visiwa ambavyo vinapatikana katika ziwa Chad kwenye mpaka na Nigeria. Eneo ambalo ni vigumu kutoa ulinzi.
Karibu na eneo hilo, kijiji cha Bosso kimekuwa kikishuhudiwa mara kwa mara mashambulizi ya hapa na pale tangu Boko Haram iliposhambulia kijiji hicho Februari 6 mwaka huu.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni