Magaidi wa Boko Haram
Magadi wa kundi la Kitakfiri la Boko Haram wameuteka
tena mji ulioko mpakani wa Marte kaskazini mwa Nigeria. Gavana na jimbo
la Borno anasema kuwa magaidi hao wameudhibiti kabisa mji huo na kusema
kuwa hilo ni pigo kubwa kwa jeshi la Nigeria. Mji huo wenye umuhimu
mkubwa kiuchumi kwa eneo la kaskazini mwa Nigeria uko katikati ya njia
ya kibiashara inayotoka Cameroon na Chad. Marte umebadilisha utawala
kutoka kwa majeshi ya serikali na magaidi wa Boko Haram mara kadha tokea
mwaka wa 2013 hadi sasa.
Wakati huo huo watu saba walipoteza maisha
jana baada ya msichana mdogo aliyekuwa amejifunga mabomu mwilini
kujilipua mjini Damaturu katika jimbo la Yobe kaskazini mwa Nigeria.
Watu wengine 31 wamejeruhiwa katika mlipuko huo uliojiri ndani ya kituo
cha basi. Maafisa wa usalama wanasema msichana aliyetekeleza hujuma hiyo
alikuwa na umri wa miaka 12.
Kwingineko imearifiwa kuwa magaidi wa Boko
Haram wanatoa mafunzo kwa wasichana 600 ili watekeleze hujuma za
kulipua mabomu kwa kujitoa muhanga katika mji mkuu wa jimbo la Borno,
Maiduguri. Naibu Gavana wa jimbo hilo Alhaj Zannah Mustapha amesema ili
kukabiliana na hali hiyo sheria za kutotoka nje zitaendelea kutekeleza
katika jimbo hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni