Jumamosi, 10 Januari 2015

DR MAGUFULI AHUDHURIA MAIISHI YA FIDEL CASTRO RAILA ODINGA

Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mfiwa, Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Mh. Raila Odinga wakiongozana kuelekea sehemu maalum ya kuaga mwili wa Marehemu Fidel Odinga kabla ya kuzikwa kwake.
Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Pombe Magufuli akishiriki ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Fidel Odinga kabla ya kuzikwa kwake. Kushoto ni Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Mh. Raila Odinga ambaye ni baba wa Marehemu.
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Mh. Raila Odinga ambaye ni baba wa Marehemu akimuombea mwanae.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli yupo nchini Kenya akiiwakilisha Tanzania kwenye mazishi ya mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya,Mh. Raila Odinga aitwaye Fidel Odinga aliyefariki mwishoni mwa wiki iliyopita. Mazishi hayo yanafanyika huko Bondo, Kisumu, Kenya leo. (TK)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni