Polisi
nchini Ufaransa wamesema kuwa wanawasaka washirika wa mhusika wa
shambulizi la kigaidi Amedy Coulibady aliyeuawa katika majibizano ya
risasi na polisi katika supermarket jana ijumaa. Hata hivyo polisi
wamemtaja Hayat Boumeddiene kuwa miongoni mwa watu hatari katika kundi
hilo la magaidi.
Harakati za kuwaokoa mateka katika Jengo hilo la
maduka kulifanyika huku ikidaiwa na vyombo vya usalama kuwa kulikuwa na
milio ya risasi katika mji mwingine Kaskazini Mashariki mwa Paris.Ndugu wawili Said na Cherif Kouachi walioendesha mashambulizi siku ya jumatano dhidi ya gazeti la Charlie Hebdo waliuawa wakati wakikimbia kutoka katika jingo huku wakijibishana risasi na Polisi.
Mwendesha mashitaka wa Polisi anasema kuwa watu watano wanaotuhumiwa kuhusika katika shambulizi hilo wanashikiliwa na Polisi.
Watu 17 waliuawa katika shambulio hilo,huku idara ya usalama ikibaini kuwa kulikuwa na mawasiliano ya simu mara 500 mwaka jana, ambapo makundi tofauti ya magaidi hao walikuwa wakipanga njama zao
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni