Ijumaa, 31 Januari 2014

MOROGORO WATEKETEZA NYAMA YA NG'OMBE NA SAMAKI


Picha ya nyama iliyoharibika baada ya kukamatwa mjini Morogoro.
 
Watumishi wa afya Manispaa ya Morogoro wamekamata nyama na samaki waliooza kilo 80 katika maduka ya bidhaa hiyo baada ya operesheni ya kushtukiza ya ukaguzi na ukamataji wa vyakula maeneo mbalimbali Morogoro.
 
Zoezi kama hili ni muhimu kuwa endelevu kwa manufaa ya afya za wana Morogoro kwa sababu watu wenye tamaa ya utajiri wa haraka haraka watatufikisha pabaya. Tunawahongeresha sana mabwana afys Morogoro. (TK)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni