Marehemu Steven Kanumba alifariki majira ya saa nane usiku,mnamo mwaka 2012 baada ya kutokea mzozo kati yake na Elizabeth Michael ambaye inaaminika kuwa walikuwa na uhusiano wa Kimapenzi.
Kanumba, ambaye alijizolea umaarufu mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati na hadi Afrika Magharibi baada ya kuwashirikisha katika filamu zake baadhi ya wasanii maarufu wa kutoka Nigeria akiwemo Mercy Johnson na Noah Ramsey.
Marehemu ambaye alizaliwa mwaka 1984, alianza kujipatia umaarufu mwanzoni mwa mwaka 2000 wakati huo akiigiza katika michezo ya runinga kupitia kundi la maigizo la Kaole Sanaa.
Aliendelea na kuigiza filamu nyingi ambazo zilimpatia umaarufu mkubwa kiasi cha kusafiri mara kadhaa nchi za nje, ambako alitambulika kama mmoja wa wasanii wenye vipaji vikubwa ambaye aliitangaza fani ya filamu nchini Tanzania maarufu kama 'Bongo Movies.'
Mazishi yake yalichukua sura ya kitaifa kutokana na umaarufu aliojijengea msanii huyo katika jamii ya watanzania na hata nchi za nje.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni