Jumapili, 26 Aprili 2015

KIONGOZI WA UPINZANI NCHINI BURUNDI ATEKWA NYARA

 
Polisi wakabiliana na waandamanaji nchini Burundi kufuatia tangazo la rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu wa urais.

Mbunge wa zamani katika bunge la Afrika Mashariki Francois Bizimana ameripotiwa kutekwa nyara siku ya jumapili mjini Bujumbura na watu wanaoshukiwa kuwa na uhusiano na serikali.
Bizimana ni miongoni mwa viongozi wa upinzani nchini Burundi ambao wanampinga rais Pierre Nkurunziza katika harakati zake za kuwania muhula wa tatu.
Mwandishi wa BBC Robert Kiptoo anasema kuwa vyombo vya habari vinaripoti kuwa kiongozi huyo wa upinzani alitekwa na watu waliojihami kwa silaha. Washirika wake pia wamekamatwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni