Alhamisi, 21 Mei 2015

NIGERIA: Taarifa ya mgahawa sio za kweli

Tunaomba radhi kutokana na taarifa ambayo tuliichapisha hapa kuhusu mkahawa mmoja nchini Nigeria.Taarifa hiyo haikuwa sahihi na ilichapishwa bila kuzingatia utaratibu wa BBC. Tumeiondoa taarifa hiyo kwenye mtandao na tayari tumeanza uchunguzi kuthibitisha ni nini kilichosababisha taarifa kama hiyo kuchapishwa.
Tunazingatia kwa thamani kubwa sifa ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC kama Idhaa inayozingatia uhakika wa habari zake na msimamo wa kutoegemea upande wowote na ni kwa sababu hiyo tunachukua hatua stahiki kuhakikisha kosa kama hilo halifanyiki tena

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni