SERIKALI
imetangaza neema kwa watumishi wa umma 4,812 baada ya jana kubainisha
kuwa kuna fursa za mafunzo 659 zitakazotolewa na Serikali ya China.
Fursa
hizo za mafunzo zimejikita kwenye maeneo ya kipaumbele cha taifa
yaliyoainishwa katika Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21).
Katika
mkutano wake na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari na
Elimu ya Bunge mjini hapa jana, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma, Dk. Laurean Ndumbaro, alisema mafunzo yamejikita
kwenye uhandisi wa viwanda, mawasiliano na usafirishaji.
Dk. Ndumbaro pia alisema mafunzo hayo yatajikita kwenye kilimo, elimu, afya, biashara na uchumi, Tehama na utawala bora.
Alisema
gharama za mafunzo hayo zitagharamiwa na Serikali ya Watu wa China
kuanzia usafiri wa ndege kwenda na kurudi, malazi, chakula na ada.
"Serikali,
waajiri watatakiwa kuwawezesha watumishi walio chini yao kuomba na
kuhudhuria mafunzo hayo kulingana na sheria, kanuni na taratibu za
utumishi," alisema Dk. Ndumbaro.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni