Gogo akiwa darasani na wanafunzi wenziwe.
Akiwa na umri wa miaka 90 mwanamke wa Kenya ambaye anahudhuria masomo
akiwa na wajukuu zake wapatao sita inaaminika ndiye mwanafunzi mzee
zaidi anayesoma shule ya msingi duniani.
Akiwa ameketi dawati la mbele kabisa darasani ,yuko darasa la tano na
amevalia nguo za shule , Priscilla Gogo Sitienei anamsikiliza mwalimu
anayefundisha kwa makini hukua akiandika majina ya wanyama kwa
kiingereza kwenye daftari lake.
Prissilla alijiunga na shule hii ya Leaders Vision Preparatory School
miaka mitano iliyopita lakini pia aliwahi kuwahudumia wakaazi wa kijiji
chake cha Ndalat kilichoko kwenye bonde la ufa kama mkunga miaka sitini
na mitano iliyopita.
Darasani Priscilla anawasaidia wengine wafanye vyema ambao wana umri
kati ya miaka 10 hadi 14 na mar azote huwaambia ujumbe wake hasa mabinti
kuwa elimu ndiyo urithi wao.
Priscilla anajulikana kama Gogo maana yake bibi katika lugha ya jamii
ya wakalenjini,anasefurahia masomo akiwa na umri wa miaka 90 katika
umri huo anajua kuandika na kusoma pia fursa aliyoikosa alipokuwa mdogo.
Lugha ambayo Priscilla anajiona yuko huru kuitumia ni lugha mama
kwake ki Kalenjin kuliko kiingereza,pindi anapotakiwa kujieleza kwanini
aliamua kujiunga na shule katika umri wake.
Sababu kubwa ambayo amekuwa akiitoa,ni ajue kusoma ili amudu kusoma
bibilia,lakini pia kwa umri wake anataka awahamasishe watoto kupata
elimu,kwani anawaona watoto wengi wakiwa hawako shuleni na watoto hao
wana watoto.
Gogo apitapo mitaani haoni shida kukabiliana na watoto ambao hawako
shuleni katika muda wa masomo na kuwauliza kwanini hawako shuleni.
Gogo anasema watoto hao humjibu kwamba hawaendi shule kwakuwa umri
wao ni mkubwa,name huwaambia mimi ni mkubwa sana kwenu lakini niko
shuleni hivyo nanyi jiungeni na shule.
Kikubwa kinachomuumiza Gogo ni kuwaona watoto wengi waliopoteza
muelekeo,wengi wao hawana baba na wanazurura hovyo mitaani,bila msaada
wowote.kutokana na hali hiyo nataka kuwahamsisha waende shuleni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni